Mwanafunzi UDSM aliyetekwa apatikana akiwa hajitambui... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa
Abdul Nondo ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu.
Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe, baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search