Mwigulu akabidhi mabati 210, mifuko ya saruji 100.... soma habari kamili na matukio360....#share
Na Mwandishi Wetu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametoa mabati 210, mifuko ya saruji 100 na sh milioni 1.5 kwa ujenzi wa Zahanati na mabweni ya wanafunzi Kata ya Mtoa, Iramba mkoani Singida
Waziri Mwigulu akikabidhi mabati kumalizia ujenzi wa zahanati
Lengo ni kusaidia na kupunguza adha wanayopata wananchi ambao inawalazimu kuvuka mto mkubwa kufata huduma ya afya umbali wa zaidi ya kilomita kumi.
Waziri Nchemba amesema jengo la zahanati limekaa muda mrefu bila kumaliziwa hivyo shilingi milioni 1.5 ni kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze na ukamilike ndani ya mwaka huu na kianze kutoa huduma.
Dk.Nchemba amesema hayo akiwa ziarani katika Kata ya Mtoa, Kijiji cha Masiga kitongoji cha Kisaki Jimbo la Iramba Magharibi Mkoa wa Singida kutekeleza ahadi alizozitoa wakati anagombea mwaka 2015.
Amesena nyakati za masika baadhi ya maeneo ni ngumu magari kufika kutokana na mito kujaa maji na barabara kuwa na utelezi na kufanya gari au watu kushindwa kupita kufuata huduma.
"Ninekerwa na jengo kukaa muda mrefu hivi,hatulali hata sekunde tunaendelea kutafuta mbao na bati nyingi zikafunike baadhi ya vituo kwa hiyo ninapoona jengo lipo hivi wala mtu asidhanie nafurahie jengo libaki vile,"amesema Dk. Mwigulu
Wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment