NACTE yafungia udahili vyuo 163...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limevifungia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada, baada ya kukutwa na upungufu ikiwamo kutokuwa na walimu wenye sifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte Dk. Annastella Sigwejo, amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kufanya uhakiki kwa vyuo 459 ambapo kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.
"Kutokana na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.”
Amesema licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459.
Nacte wanawashauri wanafunzi kuhakikisha wanajiridhisha kuwa wanaomba kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo.
Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Twaha Twaha amesema kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwenye tovuti ya Nacte.
"Hivyo Nacte inashauri waombaji wa udahili kujiridhisha kwa kuangalia hiyo orodha iwapo chuo anachokitaka kinaruhusiwa kudahili,"amesema Twaha.
No comments:
Post a Comment