Mwalimu mbaroni kwa kumkashfu Magufuli...soma habari kamili na matukio360...#shar

Na Mwandishi Wetu, Kagera

MWALIMU wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera Deogratias Simon (34) anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu rais John Magufuli.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom 

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo amekuwa akitumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na rais Magufuli kwa kumuita dikteta na mminyaji wa demkrasia.

"Mwalimu huyu tunashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia," aemsema Kamanda Ollom.

Aidha amesema kwa kuwa yupo mikononi mwao watahakikisha vyombo vya sheria vinatenda haki stahiki dhidi yake ambapo Kamanda amewataka wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi na washughulikiwe

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search