Nape: Mwenyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi
MBUNGE wa Mtama kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye amesema Mwenyezi Mungu alimuokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama
wasiopenda haki.
Amesema hay oleo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa leo ni
mwaka mmoja tangu alipotolewa bastola wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa
habari nje ya Hoteli ya Protea muda mfupi baada ya kutenguliwa nafasi yake kama
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Nape ameandika, “mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwenyezi Mungu aliniokoa na
mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi.”
Katika ujumbe huo Nape ameweka picha yake ya video akizungumza
na waandishi wa habari nje ya hoteli hiyo kueleza masuala mbalimbali, huku
akiwataka vijana kudai haki zao bila woga.
Mtu aliyemtishia bastola Nape alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao
kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini
mbunge huyo aligoma na ndipo (mtu huyo) aliporudi nyuma na kuchomoa bastola
kutoka kiunoni kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwezake.
Baada ya tukio hilo watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi
baadaye.
Kufuatia tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba alisema mtu aliyemtishia bastola Waziri huyo wa zamani wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo hakuwa askari wa Jeshi la Polisi.
Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi!
No comments:
Post a Comment