Majaliwa awataka wakazi Ruangwa kuipandisha ligi kuu Namungo FC...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Ruangwa
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa washirikiane
kuhakikisha ndoto ya timu yao ya mpira wa miguu ya Namungo FC ya kucheza ligi
kuu inatimia.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Amesema timu hiyo limeupa mkoawa
Lindi na wilaya hiyo heshima kubwa imepanda imepanda daraja kutoka ligi daraja
la pili kwenda daraja la kwanza katika msimu wa 2018/2019.
Waziri Mkuu ameyasema leo
(Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa wilaya hiyo kwenye
eneo la Namungo na kuwaomba waendelee kuisaidia timu hiyo ili iweze kupanda na
kucheza ligi kuu.
Amesema daraja la kwanza
linaushindani mkubwa zaidi, hivyo ameutaka uongozi wa timu hiyo kutumia siku
120 zilisalia kabla ya kuanza kwa ligi kwa kufanya maandalizi ya kuisuka timu
hiyo kabla ya kuanza mashindano.
“Lazima timu yetu ya Namungo FC
icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana
kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”
Pia Waziri Mkuu amekagua eneo la
ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wilayani Ruangwa unaojengwa katika kitongoji
cha Mtichi kata ya Nachingwea ambacho kinatarajiwa tumiwa na timu ya Namungo
FC.
Awali, Mwenyekiti wa timu hiyo
Bw. Hassan Kungu amesema Namungo FC imefanikiwa kupanda daraja na sasa
inashiriki ligi daraja la kwanza na malengo yao ni kuhakikisha inafanya vizuri
ili iweze kucheza ligi kuu.
“Mbali na mafanikio hayo, timu
yetu ya Namungo FC inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa
uwanja wenye viwango vya kuweza kucheza mashindano hao pamoja na chombo cha
usafiri.”
Akizungumzia historia ya Namungo
FC, Bw. Kungu amesema timu hiyo ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya
dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya
mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini.
No comments:
Post a Comment