Waziri azindua duka jipya la Tecno - Samora...soma habari kamili na matuki0360...#share

Kampuni ya simu za
mkononi, TECNO inayofanya kazi chini ya TRANSSION HOLDINGs imezidi kutanuwa
wigo wa soko la simu nchini kwa kufungua duka jipya
maarufu “Experience Center’’ Dar es salaam, Samora,
jumamosi 24/03/2018, uzinduzi huo ulihudhuriwa na naibu waziri
mawasiliano na uchukuzi mheshimiwa Atashasta Nditiye, watu maarufu, wageni
waalikwa, wadau wa TECNO kutoka mtandaoni na nyanja mbalimbali nchini.
Mgeni rasmi Naibu waziri
mawasiliano na uchukuzi Mheshimiwa Atashasta Nditiye alishiriki zoezi la kukata
utepe pamoja na mkurugenzi mkuu wa TECNO Bwana Xu pamoja na meneja wa Clouds
media group Ruge Mutahaba
Mheshimiwa pia aliweza
kuzunguka sehemu mbalimbali za duka hilo kujionea huduma mbalimbali
zinazopatikana,ni wazi TECNO imekua chachu ya kukuza Teknolojia na mawasiliano
ambapo aslimia 94 ya wananchi wana mawasiliano nchini, lakini napongeza kitendo
cha watumiaji kupewa elimu ya namna ya kutumia simu janja kuepuka uhalifu,
nawapongeza sana TECNO ”alisema Naibu waziri Nditiye.
Akizungumza na waandishi
wa habari Mkurugenzi wa TECNO nchini, Daniel Xu alisema “Ni furaha kujumuika
nanyi katika uzinduzi wa duka la TECNO “Experience Center”, wateja watapata
fursa ya kununua bidhaa, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi,sifa na
mifumo mbalimbali ya simu, lakini pia huduma ya matengezo “after sales service”
kupatikana papo hapo dukani.
Uzinduzi huu unatoa
fursa nyingine ya ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuwainua kiuchumi, ambapo
zaidi ya vijana 500 wa kitanzania wameshaajiliwa kwenye kampuni ya
TECNO,Mkurugenzi Xu alimaliza.
Pia sherehe hzio
zilipata ugeni kutoka kwa wanamuziki na mastaa tofauti tofauti ikiwemo
mchekeshaji almaarufu kama JayMondy, ambapo alijuimika na wadau wa TECNOkupitia
kurasa zake za mtandaoni. Kulikua na michezo, elimu na burudani kabambe na
bahati nasibu.
Naibu waziri Nditiye
akiendesha zoezi la bahati nasibu,na baadaye alikabidhi zawadi kwa wateja
waliojishindia zawadi kabambe kupitia droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa kwa
hisani ya TECNO.
Naibu waziri Mh. A.
Nditiye, Mkurugenzi wa TECNO na meneja masoko Franck Luo, wakiwa na baadhi ya
washindi wa bahati nasibu.
No comments:
Post a Comment