Polisi Dar wamshikilia Mnyika, Heche ... soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Katibu Mkuu Dk Vincent Mashinji.
VIONGOZI watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioripoti leo Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.
Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Katibu Mkuu Dk Vincent Mashinji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.
Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.
Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
No comments:
Post a Comment