CUF waendelea kupambana mahakamani..... soma habari kamili na matukio360...#share

TAARIFA KWA UMMA Leo Machi 22, 2018
KUHUSU MASHAURI YALIYOPANGWA KUSIKILIZWA LEO MBELE YA MHE.JAJI DYANSOBERA.
Maalim Seif Sharif kushoto na Profesa Ibrahim Lipumba kulia
Maalim Seif Sharif kushoto na Profesa Ibrahim Lipumba kulia
LEO MBELE ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera ilipangwa kutajwa, kusikilizwa na kutolewa maamuzi mashauri matano (5) yafuatayo;
1. Mashauri Namba 28, 68, na 80 yote ya mwaka 2017 yanahusu Wizi wa fedha za Ruzuku ya Chama uliofanya na Lipuma akishirikiana na Msajili Jaji Mutungi.
2. Shauri Namba 21/2017 linahusu Wabunge 19 wa CUF dhidi ya Lipumba na wenzake. Kuiomba Mahakama Kuu kumzuia Lipumba kufanya mambo ya hovyo kinyume na Katiba ya CUF.
3. Shauri Namba 13/2017 linahusu Ally Salehe [Mbunge wa Jimbo la Malindi-Unguja, Zanzibar] dhidi Bodi Feki ya Lipumba na wenzake, RITA, Jaji Mutungi na Mwanasherisa Mkuu wa Serikali.
Mashauri hayo yaliitwa Mbele ya Jaji Dyansobera na Mawakili wa pande zote walikuwepo Mahakamani.
Kutokana na Mhe Jaji kuuguliwa na Mkewe ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mhe Jaji na mawakili wakajadiliana namna nzuri ya kuweka ratiba ya kuyasikiliza mashauri yote hayo na ikaonekana kuwa kutokana na seminar ya Majaji inayoanza Kesho Mjini Arusha.
Mahakama Kuu imepanga kuyasikiliza Mashauri yote hayo mfululizo kwa siku tatu kuanzia Tarehe 16, 17, na 18 April, 2017. Na baada ya hapo itapangwa Tarehe ya kwenda kusikiliza Maamuzi [RULING/JUDGMENT] mhe Jaji amewataka pande zote zijiweke tayari na kufika kamilikamili kwa siku hizo ili mashauri hayo yaweze kufika mwisho.

AIDHA, Shauri la Msingi Namba 23/2017 kuhusu Uhalali wa Uenyekiti wa Lipumba ambalo lilikuwa Mahakama ya Rufaa Tayari lisharejeshwa Mahakama Kuu na limepangwa kutajwa Tarehe 19/3/2017 mbele ya Mhe Jaji Ignus Paul Kitusi.
WAKATI HUOHUO ndani ya mwezi huu wa Machi; Tarehe 27/3/2017 kutakuwa na Mashauri mawili Namba 557 na 558/2017 mbele ya Mhe Jaji Muruke, yaliyofunguliwa na Mhe Shaweji Mketo na Juma Nkumbi [Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa] dhidi ya Lipumba na wenzake, RITA na Wenzake juu ya KUHOJI uhalali wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini FEKI iliyoteuliwa na Lipumba na kuidhinishwa na RITA. [kesi hii inafanana na ile ya Ally Salehe] na imefunguliwa kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Wadhamini (The Trustees’ Incorporation Act Cap. 318), kifungu cha (27) kama kilivyonukuliwa hapa:
"27. Appeal
Tunatoa wito kwa Wapenzi wa CUF na Wapenda Mabadiliko wote kuendelea kuwa na SUBRA ni imani yetu kuwa MAHAKAMA ITATENDA HAKI KWA MUJIBU WA SHERIA.
THE NEW, STRONG, AND VIBRANT CUF IS COMING BACK SOON
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa Leo Tarehe 22/3/2018 na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment