Tetesi za soka Ulaya leo Ijumaa.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Mshambuliaji wa zamani wa Romania Adrian Mutu, aliyecheza chini ya Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea, amedai kwamba si kweli kuwa Ibrahimovic ameumia. Amesema ukweli ni kwamba hachezeshwi katika Manchester United kwa sababu alizozana na Mourinho. (Telekom Sport - kwa Kiromania)

Ibrahimovic
Arsenal wanapanga kumpa kiungo wa kati kutoka Misri Mohamed Elneny, 25, mkataba mpya. (Mirror)
Pasipoti ya Danny Ward ilipotea alipokuwa anawasilisha ombi la viza ya kwenda China. Kipa huyo wa Liverpool mwenye miaka 24 hivyo basi hataweza kusafiri na timu ya Wales kucheza michuano ya Kombe la China. (Times)
Juventus wamekutana na mawakala wa Anthony Martial, 22. Klabu hiyo ya Italia inataka sana kumnunua mchezaji huyo Mfaransa anayechezea Manchester United. (Premium Sport - in Italian)
Chelsea wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Wales anayechezea Arsenal Aaron Ramsey, 27, ambaye amesalia na mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake wa sasa Gunners. Ramsey bado hajatia saini mkataba mpya. (Mirror)
Barcelona wanaamini Andres Iniesta ataihama klabu hiyo na kujiunga na klabu moja Uchina mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 33 utakapomalizika mwisho wa msimu. (Sport)
Chelsea wana wasiwasi mkubwa kwamba Eden Hazard na kipa wao Thibaut Courtois wanaweza kumfuata meneja wao Antonio Conte katika kuihama klabu hiyo iwapo Blues hawatafanikiwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Wawili hao wamekuwa wakitafutwa na Real Madrid kwa muda. Paris St-Germain wa Ufaransa pia wanawafuatilia wawili hao kwa karibu. (Mirror)
Real Betis wanaamini kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere alitoa matumaini kwamba angehamia kwao ili kupata nafasi nzuri ya kujadiliana mkataba mpya na Gunners. (Sun)
Manchester United walifuta ziara ya wachezaji wa klabu hiyo kwenda kuhudhuria Tamasha ya Cheltenham Festival baada ya klabu hiyo kuondolewa kutoka Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne. (Independent)
Wamiliki wenza wa West Ham David Sullivan na David Gold wanakusudia kuhudhuria mechi ijayo ya nyumbani ya klabu hiyo licha ya kwanza mashabiki wa timu hiyo walizua fujo katika uwanja huo wa London wiki iliyopita. (Sun)
Walinzi watano walijeruhiwa na mashabiki wa Marseille waliokuwa wamesafiri Uhispania kwa mechi ya Europa League Alhamisi dhidi ya Athletic Bilbao. (El Periodico)
Mashabiki sugu kati ya 100 na 150 wa klabu ya Lyon ya Ufaransa waliwashambulia polisi nje ya uwanja wa klabu hiyo kabla ya mechi yao ya Europa League Alhamisi dhidi ya CSKA Moscow. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanataka mchezaji wa zamani wa Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid Xabi Alonso, ambaye kwa sasa amestaafu, afungwe jela miaka minane unusu kwa kosa la kutumia ulaghai wakati wa kulipa kodi. (El Mundo - kwa Kihispania)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search