Roli la mafuta lateketea, wawili wafariki.... soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu
WATU wawili wamefariki dunia baada ya roli la mafuta walimokuwamo  kuanguka na kuteketea kwa moto.
Baada ya tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio ilipotokea ajali hiyo  katika mlima sekenke njia kuu ya magari kutoka Singida kwenda Tabora.
Mabaki ya roli la mafuta lililoteketea kwa moto leo

Waziri Mwigulu amefika kuangalia jinsi ajali ya gari hilo la mafuta lilivyoanguka na kuwaka moto na kusababisha vifo hivyo ambao miili imeungua  kiasi cha kutotambuliwa hadi sasa huku jitihada zinaendelea kuwatambua.

Kwa mujibu wa shuhuda Edward Lameck, 16,aliyekuwa anapita eneo hilo amesema gari hilo lilifeli break na matairi ya mbele kuanza kuwaka moto hali iliyosababisha gari hilo kutumbukia bondeni na kuwaka moto.
Waziri Mwingulu akiangalia jinsi ajali ulivyoteketeza roli la mafuta

Inaelezwa kuwa imeshindikana watu hao kuokolewa  kutokana na moto mkubwa uliokuwa unawaka. Juhudi zinaendelea kutambua mmiliki wa gari ili kufahamu waliokuwa kwenye gari hilo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search