Samia ateta na mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Bill na Milinda Gates Faundation...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan leo  amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates Foundation Rodger Voorhies kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates, Rodger Voorhies kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Samia amesema wamezungumza mambo mengi na Rodger hasa kwenye masuala ya afya, uwezeshaji wanawake kiuchumi, kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza kwenye kilimo biashara lakini pia kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.

"Tumezungumza namna ya kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake wakulima ikiwa pamoja na uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata mikopo," amesema Samia.

Pia amezungumzia suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama haswa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya magojwa ya kipindu pindu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates Foundation Rodger Voorhies amesema wamekuja kwa Makamu wa rais kuzungumza juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo hapa nchini haswa katika masuala ya Kilimo na Afya na Mkakati Mpya wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake katika masuala yanayohusu Fedha.

Mkurugenzi huyo ameahidi ushirikiano mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa miradi ya taasisi yao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search