Watano wafariki, wengine wajeruhiwa katika ajali Morogoro...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Morogoro
WATU watano, wanawake wanne na mwanaume mmoja wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha basi la New force T 346 DLY iliyokuwa ikitokea Dar kuelekea Tunduma na Hiace T 962 BSE iliyokuwa ikitokea kijiji cha Mlali kuelekea mjini Morogoro.
Ajali hiyo imetokea jana saa 4.15 asubuhi eneo la Lungenba, kilometa chache kutoka Msamvu kuelekea Iringa.
RTO wa mkoa wa Morogoro Boniphace Mbao amesema majeruhi wa ajali hiyo ni 12 ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Chanzo cha ajali ni dereva wa Hiace kujaribu kuyapita magari mengine bila tahadhali na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo. Dereva wa Hiace amepoteza maisha.
Picha mbalimbali za ajali iliyotokea leo Mkoani Morogoro ikihusisha gari la Kampuni ya New Force na gari dogo aina ya Hiace
No comments:
Post a Comment