Al Masry watua kuikabili Simba....soma habari kamili na matukio360...#share

Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Wapinzani
wa Simba katika kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Al Masry kutoka Misri
tayari wamewasili kwenye ardhi ya Tanzania kwa mapambano ya kutafuta nafasi ya
kuingia 16 bora ya Michuano hiyo.
Siku ya Jumatano ya Marchi 7 wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa
kwenye uwanja wao Taifa jijini Dar es salaam kucheza na Al Masry kutoka Misri
mchezo ambao unatarajiwa kuwa mzuri na mgumu kwa pande zote mbili kutokana na
ubora wa vikosi vyote.
No comments:
Post a Comment