Samia aagana na mabalozi wa Tanzania nchini Rwanda, Urusi...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MABALOZI wa Tanzania Nchini Rwanda Ernest Mangu na Meja Jenerali Mstaafu Simon
Marco Mumwi wa Urusi leo wamekutana na kuzungumza na Makamu wa Rais
wa Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma.
Mabalozi hao walifika kwenye makazi
ya Makamu wa Rais, Kilimani Dodoma kwa lengo la kumuaga ,walimuahidi
Makamu wa Rais kufanya kazi kwa ajili ya Tanzania.
Wamemuambia Makamu wa Rais
wanajua dhamana kubwa waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli na dhamira yake ya Tanzania ya Viwanda .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi
wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi pamoja na
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu ambao walifika nyumbani kwa
Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma.
Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment