Serikali yafafanua kuhusu watanzania nchini Oman.... soma habari kamili na matukio360...#share

TAARIFA YA UFAFANUZI
KUHUSU RAIA WA TANZANIA NCHINI OMAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga
Kuna kipande cha video kinasambaa mitandaoni kikiwa na maelezo kuwa raia
wa Tanzania wanaoishi nchini Oman wamekusanyika ofisi ya Ubalozi kushinikiza
kurejeshwa nyumbani kutokana na mateso na adhabu kali
wanazopata kutoka kwa mabosi wao.
wanazopata kutoka kwa mabosi wao.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, baada ya kutazama
kipande hicho cha video iliwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kwa
madhumuni ya kujua usahihi wa jambo hilo.
balozi ulitoa ufafanuzi kuwa uliandaa mkutano wa Watanzania wote wanaoishi
Oman na ulipangwa kufanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Muscat tarehe
23 Machi 2018. Matangazo ya mkutano huo yalitaka Watanzania watakaopenda
kushiriki wajisajili kabla ya siku ya mkutano.
Watanzania takriban 200 walijisajili na ubalozi ulifanya maandalizi yaukumbi,
vyakula na vinywaji kwa ajili ya watu 300 kwenye hoteli ya GoldenTulip.
Siku ya mkutano ilipowadia, Watanzania zaidi ya elfu moja walijitokeza
na kusababisha ugumu wa kuendelea na mkutano kutokana na maandalizi yaliyofanywa
yalilenga watu 300.
Kamati ya maandalizi ilipoona ukumbi umejaa na watu walio nje ni weng mara
mbili zaidi ya watu waliokuwemo ndani ya ukumbi iliamua kufunga milango na
kuwaomba waliochelewa warejee nyumbani.
Uamuzi huo haukuwafurahisha watu waliochelewa, hivyo walishinikiza waingizwe
kwenye ukumbi wa mkutano, kitendo ambacho kiliashiria uwezekano wa kutokea
vurugu kubwa.
Kutokana na uhalisia huo, Kamati ya maandalizi ambayo ilijumuisha pia viongozi
wa Watanzania wanaoishi nchini humo ilishauriana na kuamua kuwa mkutano huo
uahirishwe na maandalizi yaanze upya kwa madhumuni
ya kupata ukumbi na huduma nyingine zitakazokidhi idadi kubwa ya watu.
ya kupata ukumbi na huduma nyingine zitakazokidhi idadi kubwa ya watu.
Kutokana na ufafanuzi huo, Wizara inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania
kuwa kipande hicho cha video kimechukuliwa wakati Watanzania wanashinikiza
kuingia kwenye ukumbi wa mkutano na sio kwamba wamekusanyika kwenye ofisi ya
ubalozi wa Tanzania kushinikiza kurejeshwa nyumbani kutokana na mateso
wanayoyapata.
Imetolewa na: Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dar es Salaam, 26 Machi, 2018
No comments:
Post a Comment