Uvccm wamchokonoa Waziri Mwakyembe.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Kheri Jemes amewataka viongozi wenye mamlaka ya kusimamia tasnia ya sanaa na
utamaduni nchini kuacha kufanya kazi ya uhakimu.
Kauli hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kusitisha kuchezwa kwa nyimbo 15 za wasanii mbalimbali kwa kile kilichodaiwa ni nyimbo hizo kutokuwa na
maadili ya kitanzania.
Akizungumza jana mjini Dodoma na wanachama wa umoja huo, James amewataka
viongozi wenye mamlaka hayo kuwaelimisha wasanii nini cha kufanya ili
kuboresha badala ya kufungia tu.
“Viongozi wanaoshughulika na masuala ya sanaa na utamaduni wasiifanye kazi hii kama kazi ya uhakimu bali waifanye kama kazi ya ualimu kwa kuwafundisha watu namna ya kufanya”- amesema James.
“Serikali ya CCM imeahidi ajira kwa vijana, Vijana wameamua kujiajiri
kwenye sanaa. Walimu wetu ni kuwawezesha kwenye sanaa na sio kuwakatisha tamaa
kwahiyo tusitumie kigezo cha sheria na taratibu kuwaangamiza watu ambao
tungeweza kuwaelimisha na wakafanya vizuri zaidi,” ameongeza.
“Leo tuna wasanii ambao wameitangaza nchi yetu vizuri na
wanalipa kodi kwa kazi zao sasa leo tunataka kupoteza mabalozi wazuri na
walipakodi kwa makosa madogo ambayo yanaweza kurekebishwa na tukaendelea
kufanya vizuri. Kama tutaaendelea kuwaacha vijana wakiangamizwa kwa kitu
kinaitwa kanuni na taratibu za sheria basi hakuna kijana atakayebaki hapa”
Hivi karibuni Nasib
Abdul ‘ Diamond Platnum’ aki mmoja wa wahanga waliofungiwa
nyimbo, akihojiwa na kituo kimoja
cha redio nchini alimtuhumu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Juliana Shonza kufungia nyimbo za wasanii zikiwamo zake mbili za ‘Hallelujah’ na ‘Wakawaka’ bila
kuzingatia hasara na usumbufu wanaoupata wakati wakiziandaa.
No comments:
Post a Comment