SERIKALI:Ugonjwa wa figo bado tatizo nchini....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI imesema maradhi ya ugonjwa wa figo nchini yanaongezeka na tafiti zilizofanya kanda ya kaskazini mwaka 2014, zinaonesha kati ya asilimia 7 hadi 15 ya watanzania wana matatizo sugu ya figo.
Pia imesema wanawake milioni 195 wanaugua ugonjwa wa figo duniani na unashika nafasi ya nane kwa kusababisha vifo huku
wanawake 600,000 hupoteza maisha kutokana na matatizo hayo f duniani kote kila mwaka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile akitoa maelekezo mbele ya Watumishi wa Umma na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya Siku ya Figo Duniani tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.
Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dk.Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko la siku ya Figo duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8.
Dk.Ndugulile amesema tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonesha wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya figo ukilinganisha na wanaume.
Amesema kwa wastani asilimia 14 ya wanawake wanaathiriwa na matatizo ya figo ukilinganisha na asilimia 12 kwa wanaume
Amesema kwa upande wa Tanzania ugonjwa huo umekuwa ukiongezeka na tafiti zilizofanya kanda ya kaskazini mwaka 2014, ulionesha kuwa kati ya asilimia 7 hadi 15 ya watanzania wana matatizo sugu ya figo.
Ameongeza kuwa kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangiwa na magonjwa ya Shinikizo la Damu na Kisukari
Hata hivyo utafiti uliofanywa na Hospitali ya Kanda Bugando, umeonesha kuwa asilimia 83 ya wagonjwa wa Kisukari wana matatizo sugu ya figo na kati ya hawa, asilimia 25 walikuwa wanahitaji huduma za usafishaji damu.
“Wagonjwa waliokuwa wanapatiwa huduma ya kusafisha damu kutokana na figo kushindwa kufanya kazi, ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walikuwa 178. Kwa sasa idadi ya Wagonjwa hawa imeongezeka na kufikia 783," amesema.
Aidha mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa sh. milioni 37 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama ya kusafisha damu.
Aidha, anahitaji kusafiri na kufika kwenye huduma kwa wastani wa safari 126 kwa mwaka sawa na wastani wa safari 3 hadi 4 kwa wiki.
Amesema Serikali imekuwa ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na idadi ya waliokwishapandikizwa figo na ambao wanafuatiliwa matibabu yao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni takribani 204.
“Gharama za kupandikiza figo nje ya nchi ni wastani wa fedha za Kitanzania milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja,ikijumuisha upandikizaji,nauli na malazi,”amesema Dk.Ndugulile
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kubadili jinsi ya kuandaa vyakula mfano kwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula na kiasi cha mafuta kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza magonjwa shinikizo la damu (hypertension), kisukari na unene wa kupindukia, vile vile kuhamasisha familia kufanya mazoezi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya figo ya mwaka huu wa 2018 ni “FIGO NA AFYA YA WANAWAKE: WASHIRIKISHWE, WATHAMINIWE NA WAWEZESHWE”.

No comments:
Post a Comment