Afisa TRA apandishwa kizimbani.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu Dar es Salaam.

Afisa Msaidi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA}, Joyce Amon (25) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kushawishi rushwa.



Wakili wa Serikali, Sophia Nyanda leo amedai mbele ya Hakimu Mkazi  Adelf Sachore kuwa  Desemba 12,2017  katika eneo la Gerezani Kariakoo Wilaya ya Ilala mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa msaidizi wa kodi  alishawishi rushwa ya Sh 800,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiweze kumwandikia cheti cha faini cha  kodi  ya ongezeko la thamani (VAT).

Katika shtaka la pili, mwanafunzi  Lilian  Wilson (23) naye anakabiliwa na shtaka la  kusaidia kutenda kosa hilo.

Wakili Nyanda alidai kuwa  Desemba 13,2017 katika hoteli ya Tansoma mshtakiwa huyo Lilian alimsaidia Joyce ambaye ni afisa msaidizi wa kodi wa TRA kujipatia  kiasi cha Sh 400,000 kutoka kwa Antelo Sanga  ili asiweze  kumpatia  cheti cha faini cha kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Sachore  alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka katika taasisi zinazotambulika kisheria  ambao watasaini ahadi ya Sh 5 milioni kwa kila mmoja. Na kwamba barua hizo zitahakikiwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la. Hadi tunaondoka eneo la mahakama walikuwa bado hawajatimiza masharti hayo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search