SERIKALI:Unyanyasaji kijinsia unaathiri tabaka zote...soma habari kamili na matukio360...#share
Na
Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI amesema ukatili dhidi ya wanawake unaathiri matabaka yote na viwango vya ukatili vya kimwili, kingono na kisaikolojia vipo juu zaidi vijijini na miongoni mwa wale wenye elimu ya chini
SERIKALI amesema ukatili dhidi ya wanawake unaathiri matabaka yote na viwango vya ukatili vya kimwili, kingono na kisaikolojia vipo juu zaidi vijijini na miongoni mwa wale wenye elimu ya chini
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP-Mtandao Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na mtandao huo.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na katibu wa
wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Sihaba Nkinga
katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na TGNP-Mtandao.
“Takwimu
zinaonesha karibu wanawake wanne kati ya kila 10 wamewahi kunyanyaswa huku asilimia
20 wakifanyiwa ukatili wa kijinsia kwenye maisha yao,” amesema Nkinga.
Amesema katika
mapitio ya ukatili dhidi ya watoto ya mwaka 2011, imeonekana mmoja katika ya
kila wasichana watatu, na mmoja katika kila wavulana saba wanapitia aina moja
au nyingine ya ukatili wa kijinsia kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Nkinga
amesema ukatili dhidi ya wanawake unaathiri matabaka yote, na viwango vya
ukatili vya kimwili, kingono na kisaikolojia vilikuwa juu zaidi vijijini na
miongoni mwa wale wenye elimu ya chini.
Amesema katika
kukabiliana na vitendo hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa mpango
wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2017/2018-2021/22
mpango ambao umekwishaanza utekelezaji wake.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP-Mtandao Lilian Liundi, amesema mada kuu katika
maadhimisho hayo kidunia ni “Sukuma Mabadiliko kuelekea usawa wa jinsi,” ambapo
msisitizo ni kutomuacha mtu nyuma yaani twende wote huku kitaifa yakiongozwa na
mada kuu isemayo “Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuimarishe usawa wa jinsia na
uwezeshaji wanawake vijijini.”
Amesema wanawake
ni mgongo wa maendeleo vijijini na uchumi wa nchi. amesema “Takwimu za UN Women
zinaonesha kuwa wanawake ni asilimia 43 ya nguvu kazi ya kilimo duniani, ambayo
kwa nchi nyingine inapanda hadi asilimia 70. Kwa upande wa Afrika kilimo
kinafanywa kwa asilimia 80 na wakulima wadogo wadogo ambao wengi wao ni
wanawake.
Amesema pamoja
na mchango mkubwa wa wanawake katika sekta ya kilimo, bado wanakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo umasikini na kutokumiliki adhi na asilimali za
uzalishaji. Takwimu zinaonesha takribani asilimia 60 ya wanawake ni masikini
hususani wale wa vijijini.
Liundi
amesema katika kusisitiza ushiriki wa wanawake katika Tanzania ya viwanda
inatakiwa kuzingatiwa kanuni (principal) ya malengo endelevu ya dunia ya
kutomwacha mtu nyuma kwa kufanya uchambuzi wa kina kwa jicho la jinsia ili
kuleta ushiriki jumuishi na wenye tija.
No comments:
Post a Comment