Tahliso waibua tena sakata kifo cha Akwilina...soma habari kamali na matukio360...#share

JUMUIYA YA
TAASISI ZA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA (TAHLISO) OFISI YA MWENYEKITI TAHLISO
TAARIFA KWA
UMMA.
Mwenyekiti wa Tahlisi George Albert Mnali wa pili
kutoka kulia akizungumza na baraza Kuu la Senate leo kushoto ni Katibu
Mkuu wa Tahliso John Mboya kulia ni Katibu wa Baraza hilo Faidhaa Msangi na
kulia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Rais wa Chuo cha Zanzibar University
Ndugu waandishi wa habari tunawashukuru sana kwa kukubali
wito wetu wakuja kujumuika pamoja na sisi.
Leo tarehe
3/3/2018 tumekuta na viongozi wa vyuo vikuu nchi nzima kwa ajili yakujadili
changamoto zinazotukabili. Kikao hiki ni cha TAHLISO BarazaKuu (SENATE) kinacho
husisha Maraisi wa serikali za wanafunzi wa VyuoVikuunchini.
Tunatambuakwambakunakifo
cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina Akwilini,mwanafunziwachuo cha NIT kilichotokea
mwezi wa pili.
Tunawashukuruwanafunziwenzetukwautulivumkubwanamshikamanowaliouoneshatangumsibaulipotokea,
wakatiwakipindi cha majonzihadikufikiasasa.
TunamshukuruMhe.Raisi
wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuingilia kati suala hili na kuagiza
uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika
kuhusika na kifo cha AkwilinaAkwilini.
Vilevile tunaishukuru
WizarayaElimu, Sayansi na Teknolojia kwa ukaribu waliouonesha katika kipindi
chote cha msiba.Tunaomba wanafunzi waendelee kuwa watulivu wakati maagizo ya
Rais yakitekelezwa.
Aidha
tunapenda jamiii tambue kuwa TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi
wote nchi nzima Tanzania na sio kikundi kingine chochote kile.
Vipo vikundi
vingivi mejitokeza na kutoa matamko mbalimbali baada ya kifo hiki kutokea,
vikundi vingine vikaenda mbali Zaidi kwa kuwataka baadhi ya watendaji wa Serikali
akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani kujiuzulu jambo ambalo linaashiria vikundi
hivyo kuongozwa ama kutumika namakundi ya kisiasa, haiwezekani kutaka watendaji
wa Serikali wajiuzulu wakati uchunguzi bado unafanyika na matokeoya uchunguzi
huo bado hayajatoka.
Tunatoa
wito kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na kutumia mwamvuli wa Marais
waVyuoVikuu kama kinga yao ili kuu hadaa Umma kwamba wanaungwa Mkono, vikundi
hivyo viache tabia hiyo vinginevyo tutawachu kulia hatua za kinidhamu.
TAHLISO
tunasubiri matokeo ya Uchunguzi unaofanyika juu ya kifo cha Akwilina na
tunaimani wahusika wote watachukuliwa hatua kali zakisheria.
Tunawaombawanafunzi
wote tuendelee kuwa watulivu wakati tukisubiri matokeo hayo na kujiepusha na
maandamano na vitendo vyovyot e vitakavyo sababisha uvunjifu wa Amani nakuleta
mgawanyo miongoni mwawanafunzi.
Hata hivyo namna bora yakufikisha hoja nikutumia njia ya majadiliano
kama wasomi badala ya kutumia nguvu ama maandamano kwakutofuata taratibu na
madhara yake ni kusababisha vuruguzi sizotakiwa na hatimaye kuhatarisha usalama
na hivyo kuathiri jamii kwaujumla wake.
Vurugu
zozote zitokanazo kwa kutozingatia taratibu zinaweza kudhorotesha shughuli za
kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Uchumiwa Taifa letu. Vile vile zinapoteza mvuto
kwawawekezaji wanje na wandani, ikiwemo shughuli za utalii nchini ambazo
zinachangia pato la Taifa letu.
Athariza
Vurugu na kukosekana kwa amani zipo wazi natunaziona kwa nchi nyingine zikiwemo
baadhi ya nchi jirani zetu ambao wamekua wakimbizi nchini kwetu kila siku.
Tunaona kuwa kama wanataaluma tunajukumu kubwa
la kuelimisha jamii na kuwamfano bora wakutumia njia za majadiliano katika
kujenga hoja zetu ilizitatuliwe kuliko kutumia njia ya maandamano au vurugu
zisizo na ulazimawowote.
Taasisi hii
ndio yenye dhamana ya kutetea nakusimamia maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo na
vyuovikuu Tanzania na si vinginevyo.
………………………………….
GEORGE
ALBERT MNALI
MWENYEKITI
TAHLISO
No comments:
Post a Comment