TECNO kuzindua toleo jipya?...soma habari kamili na matukio360....#share


Paparazi tayari wameshaanzisha uvumi kama ilivyo ada, ambapo safari hii wakiihusisha kampuni kinara katika uzalishaji wa simu za mkononi TECNO,ikitajwa zaidi midomoni mwa watu, tetesi zaidi zinaihusisha kampuni hiyo pendwa na ujio wa toleo jipya ikiwa ni muendelezo wa jamii ya Camon inayosemekana kuzinduliwa nchini Nigeria, siku na saa bado havikuwekwa wazi.
Inasemekana kwamba simu hiyo itaendana na uchumi wa Afrika ikikadiriwa kuwa na bei nafuu, hivyo nadhani wa Afrika wanacho cha kujivunia
Swali ni kwamba je ni kweli TECNO watakuja na toleo jipya kama inavyosemekana midomoni mwa wadau mbali mbali, bado hakujakuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika
Mara nyingi TECNO inapohusishwa kuhusu toleo jipya bhaasi huwa kweli,je awamu hii TECNO wanakipi cha tofauti? Maswali yamekua mengi yakiacha wadau vinywa wazi wakiwa na shauku ya kutaka kuona ni nini TECNO watakachoingiza sokoni ikiwa ni muendelezo wa Camon.

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search