Tetesi za soka Ulaya leo Jumapili.... soma habari kamili na matukio360....#share
Na mashirika ya kimataifa
Mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard, 25, atapewa mkataba mpya Old Trafford miezi 11 baada ya kusaini mkataba ulioboreshwa. (Sunday Star)
Jesse Lingard,
Kiungo wa kati wa Bournemouth Harry Arter ameachwa nje mechi sita za klabu hiyo. Mchezaji huyo wa miaka 28 hivi majuzi amehusishwa na kuhamia West Ham. (Bournemouth Echo)
Paris St-Germain wako wazi katika kumuuza mshambuliaji Neymar, 26, kwa klabu yake ya zamani Barcelona au kwa washindani wao Real Madrid. (Sky Sports)
Real Madrid watamwinda kipa ya Hajduk Split Karlo Letica 21, ikiwa hawataweza kumpata kipa wa Manchester United David De Gea,27, au kipa wa Chelsea Mblegiji. Thibaut Courtois (Marca)
Meneja wa Watford Javi Gracia hajui ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Abdoulaye Doucoure, 25, atasalia Watford licha ya Manchester United, Liverpool, Arsenal na Tottenham kuonyesha nia ya kumsaini (Watford Observer)
Liverpool wana uhakika wa kufanikisha rekodi ya pauni milioni 40 kwa kipa wa England na Stoke City wa miaka 24 Jack Butland. (Sunday Mirror)
Manchester United wana mpango wa kumtafuta beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 27, msimu ya joto. (Sunday People)
Chelsea watahitaji kumenyana na Paris St-Germain ikiwa wangetaka kumfanya meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa meneja wao.
Meneja wa Huddersfield Town David Wagner ameibuka kuwa windo la Borussia Dortmund. (Sunday People)
Meneja wa Everton Sam Allardyce anaamini kuwa mshambulizi wa Uturuki Cenk Tosun, 26 ameanza kulipa pauni milioni 27 ambazo klabu hiyo ilimnunua (Liverpool Echo)
Mshambulizi wa Liverpool Danny Ings, 25, amasema itakuwa uamuzu wa upuuzi kuondoka Anfield mwisho wa msimu. (Sunday Express)
No comments:
Post a Comment