Radi yauwa watu 16 kanisani.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
RADI imeuwa takriban watu 16 na kuwajeruhiwa wengine kadhaa kwenye kanisa moja la KiAdiventista nchini Rwanda siku ya Jumamosi

Wengi wa waathiriwa walifariki papo hapo wakati radi ilipiga kwenye kanisa katika wilaya iliyo kusini mwa nchi ya Nyaruguru, kwa mujibu wa meya wa eneo hilo, Habitegeko Francois.
Watu wawili walifariki kutokana na majeraha, na watu 140 walikimbizwa hospitalini na vituo vya afya.
Radi pia ilimuua mwanafunzi eneo hilo siku ya Ijumaa kwa mujibu wa meya.
Ajali hiyo katika eneo lenye milima karibu na mpaka na Burundi, ilitokea saa za mchana wakati waumini walikuwa bado ndani ya kanisa.
Madaktari wanasema kuwa watu wangine watatu wako hali mahututi lakini wanapata nafuu, Bw Francois aliiambia AFP.
Alisema kuwa katika kisa cha siku ya Ijumaa, radi ilipiga kundi la wanafunzi 18 eneo hilo na kumuua mmoja.
Watatu kati ya wanafunzi hao wamebaki hospitalini huku wengine wakiruhisiwa kwenda nyumbani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search