Tulia akabidhi mabati 100, mifuko ya saruji 100...soma habari kamili na matukio360...#share



Na mwandishi wetu, Mbeya



NAIBU Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa msaada wa mifuko ya saruji 100 na mabati 100 katika shule ya Sekondari Pankumbi halmashauri ya Jiji la Mbeya vyenye thamani ya Sh milioni 3.9 na amekabidhi jengo la upasuaji katika kituo cha afya ruanda Nzovwe.

Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akikabidhi msaada wa saruji mifuko 100
kwa Mkuu wa Mkoa Amos Makalla, katikati mwenye Miwani (wapili kushoto)
ni Mdau wa Elimu Ndele Mwaselela  na ( kwanza kulia)  Naibu Spika Dkt
Tulia Ackson

Msaada huo umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mdau wa maendeleo mkoa, Ndele Mwaselela


Dkt Tulia amesema msaada huo umetolewa kupitia wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kushirikiana na Taasisis ya Tulia Trust na lengo ni kusaidia serikali katika kuboresha huduma muhimu hasa elimu na afya


"Tulia Trust iko beba kwa bega na Serikali katika kuhakikisha
inaboresha huduma muhimu katika jamii ,kwa kushirikiana na mdau mkubwa wa maendeleo Mkoa Ndele Mwaselela,"amesema.


Aidha amepongeza jitihada za Makalla kwa  utaratibu wa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo shughuli za miradi ya maendeleo .

Kwa upande wake Makalla, ameuagiza uongozi wa shule hiyo na Diwani kuhakikisha misaada iliyotolewa inatumika kama ilivyokusudiwa na kwa wakati.


"Ninajua kuna baadhi ya watu misaada inapotolewa kwa ajili ya
maendeleo wanaweka na kufungia majumbani  sasa sitaki kusikia na nitarudi tena kukagua ujenzi huu," amesema.


Mkuu wa Shule hiyo, Sister Seken amesema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na thamani za ofisi za walimu na inawalizimu kutumia madawati ya wanafunzi.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search