Ujenzi nyumba za polisi Arusha wakamilika....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Arusha

UJENZI wa nyumba mpya za makazi ya askari polisi mkoani Arusha umekamilika. Hutua hiyo ilifuatia baada ya mwaka  jana moto kuteketeza nyumba zilizokuwepo eneo hilo.


Makazi mpya ya nyumba za askari polisi mkoani Arusha


Hatua hiyo imeridhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba alipokagua ujenzi wa nyumba hizo za kisasa.


Dk Mwigulu amempongeza  rais John Magufuli, mkuu wa Mkoa huo,  Mrisho Gambo na wafanyabiashara mkoani humo kusaidia ujenzi wa nyumba hizo.


"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, ili ni jambo kama waziri na mshukuru sana Rais na litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanavyofanya, " amesema Mwigulu.


Mrisho Gambo akimueleza jambo Waziri Mwigulu alipokagua ujenzi wa nyumba za askari polisi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo,  Gambo amemshukuru waziri Mwigulu kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo ikiwamo kukagua kila hatua ya ujenzi.

Pamoja na mambo mengine Mwigulu amekubali kupeleka gari la polisi katika kituo cha Murieti ili kupunguza matukio ya kihalifu kufuatia ongezeko la watu katika eneo hilo.




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search