Mauaji nchini serikali yatakiwa kutoa tamko...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

SERIKALI imetakiwa kutoa tamko dhidi ya vitendo vya kupotea na kuuawa kwa watu nchini.
Mshauri wa masuala ya jinsia, mwanaharakati wa haki za binadamu na huduma ya jamii (Tamwa) Gemma Akilimali akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Pia imetakiwa kuwa na uvumilivu kwa kuacha kuwanyamazisha watu wanaotumia uhuru wao wa kikatiba kutoa matamko na maamuzi juu ya serikali ilimradi wasivunje sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na  Mshauri wa masuala ya jinsia, mwanaharakati wa haki za binadamu  na huduma ya jamii (Tamwa) Gemma Akilimali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema vitendo hivyo ni ishara ya amani na usalama kuanza kuyeyuka nchini.

Amesema “Serikali haioneshi kuhusika na matukio haya, lakini ni kwa nini iko kimya?, Tunaamini kwamba inajua na inaendelea kujua tunaomba serikali iwajibike kutoa matamko na kufuatilia usalama wa raia ili kuwe na hiyo amani ambayo inataka kuanza kuyeyuka,” amesema Akilimali.

Amesesitiza kwa kusema kuwa serikali inatakiwa kuwajibika katika kusimamia amani, usalama na haki ya kuishi kwa binadamu ambapo ameongeza kwamba kama amani itakosekana tutakuwa tumepoteza tunu muhimu sana.

Mwanaharakati huyo amesema  kwa sasa kunaviashiria vya matukio ya kuanza kupotea amani ndiyo sababu  sauti zinaanza kujitokeza kuidai ambapo ameeleza kwamba kwa sasa kuna mmomonyoko mkubwa wa amani na hasa kutokana serikali kushindwa kusikiliza sauti za watu.

“Kwa sasa kuna tatizo linalojitokeza na kummomonyoka kwa amani na sababu ni serikali kushindwa  kusikiliza sauti na sisi huwa tunaamini sauti inaleta ajenda, unaponyamanzisha sauti unakosa ajenda,” amesema.

“Lakini vilevile matukio mbalimbali ambayo yanatokea na hasa yale yanayosababisha sasa mpaka watu kupotea ukisema hiki tayari unapotea pamoja na vifo visivyotaraiwa vinavyotokea ni hofu inayoanza kutawala nchini,” amesema.
Ametoa msisitizo kwa serikali kuvumilia wanaoikosoa kwa kusema “Kwa hiyo serikali tunaiomba ivumilie, wale ambao wanataka kusema chochote ila wasivunje sharia, kwa hiyo sisi tunaomba uvumilivu wa serikali,”

Amesema njia zianzotumia kwa sasa siyo zile abazo zilikuwa zinaendeleza amani bali ni zile ambazo zinaichokonoa amani na kwamba kama kunawatu wanakosea wanatakiwa wapelekwe mahakamani ili mahakama iweze kuamua.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search