Urusi yajaribia kombora lisiloweza kuzuiwa....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mashirika ya kimataifa
Urusi inasema imefanakiwa kulifanyia majaribio kombora lake lisiloweza kuzuiwa, moja ya makombora yaliyotangazwa na rais wa nchi hiyo,Vladimir Putin mapema mwezi huu.
Wizara wa ulinzi ya Urusi ilichapisha video ikionyesha kombora hilo likifyatuliwa kutoka kwa ndege ya vita na kuacha moshi nyuma.
Tarehe mosi mwezi huu , rais Putin alitangaza kuwa kombora la Kinzhal na la kiwango cha juu
Kombora la Kinzhal linaelezewa kuwa linaweza kusafiri mara kumi ya kasi ya sauti na linaweza kufika hadi kilomita 2,000.
Wizara ya ulinzi ilisema kuwa kombora hilo lilifyatuliwa kutoka kwa ndege aina ya MiG-31 ambayo ilipaa kutoka uwanja ulio kusini magharibi mwa Urusi siku ya Jumamosi.
"Uzinduzi huo ulienda kulingana na mpango, kombora hilo liligonga lengo lake," wizara ilisema.
Putin anatarajiwa kuchaguliwa tena kama rais wa Urusi wiki moja inayokuja.
Kama sehemu ya hotuba yake kwa taifa ya tarehe mosi mwezi hu, alicheza kanda ya video ambayo ilionekana kuonyesha mvua wa makombora katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Marekani ilijibu ikisema kwa hiyo haistahili kuwa taibia ya taifa kama Urusi.
No comments:
Post a Comment