Watano wapandishwa kizimbani..... soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu,  Dar es Salaam.

Watu watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka  ikiwamo la kuwaingiza nchini kimagendo wahamiaji haramu na kughushi vyeti vya kuzaliwa.
Watu hao ni mfanyabiashara Abdulkadir Salah (37), dereva Said Mtambo (34), kondakta Hassan Mgeni ( 41) na madalali Issa Juma na  Mohammed Ngotyagayi.


Akisoma hati ya mashtaka jana kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi, Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alidai kuwa Machi Mosi, 2018  Makao Mkuu ya Uhamiaji Temeke mshtakiwa Abdulkadir Salah aliwaingiza nchini kimagendo  Aden Ibrahim, Liban Gulet na Mohammed Ibrahim ambao ni raia wa Somaria.

Mlay alidai kuwa siku hiyo ya Machi  Mosi,2018  mshtakiwa  Salah alikamatwa akiwa nchini bila ya kuwa na hati ya kusafiria pamoja na Visa.

Mbali na mashtaka hayo mshtakiwa Salah anadaiwa kukutwa na nyaraka zilizoghushiwa ambazo ni vyeti vya kuzaliwa namba BB/NO 0094366 chenye jina la Ahmed Mursal, BB/NO 0418995 Hadija At human na BB/NO0419004 Ally Abdi kwa lengo la kupata hati za kusafaria.

Kwa upande wa washtakiwa Saidi, Hassan,Issa na Mohammed wao wanakabiliwa na shtaka la kumsaidia kuwaingiza nchini kimagendo wahamiaji haramu ambao ni raia wa Somaria.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walisaidia kuwaingiza kimagendo nchini Aden Ibrahim, Libyan Gullet na Mohammed Ibrahim.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa wote wamekana na upande wa mashtaka alidai kuwa upelelezi haujakamilika.

Hakimu Shaidi akitoa masharti ya dhamana alimtaka mshtakiwa Abdulkadir kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani ama kuwa na mdhamini ambaye ni raia wa Tanzania ambaye atawasilisha mahakamani hati ya mali isiyohanishika.

Kwa upande wa washtakiwa wote wawe na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 5milioni.

Mshtakiwa zaidi na Hassan wamekamilisha masharti hayo na kesi itatajwa Machi 28,2018.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search