Waziri aagiza mhandisi akamatwe.... soma habari kamili na matukio360....#share


Na Mwandishi Wetu, Morogoro

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameagiza vyombo vya usalama kumkamata
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Interconsult kutokana na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Gombe uliopo Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.


Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Jumuiya yaWatumiaji Maji katika Kata yaLupiro, Wilaya ya Mahenge, mkoani Morogoro.


Pia ameagiza kufanyika uchunguzi kwenye mradi huo wa Gombe ambao umechelewa kukamilika licha ya asilimia kubwa ya fedha kuwa zimeshalipwa kwa mkandarasi, lakini pia unakosa thamani halisi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wake.

Aweso ametoa maagizo hayo wakati alipokuwa ziarani katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro mara baada ya kupata taarifa ya kusuasua kwa mradi huo na wananchi wa Gombe kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.

‘‘Katika taarifa nimeambiwa kuwa mradi unatoa maji, lakini nimekuja kuona na si kweli wakati wizara imetoa fedh,”. 

“Kama Naibu Waziri wa Maji sitakubali kusikia fedha za miradi ya maji zinaliwa kila ninapoenda, naagiza Mhandisi Mshauri akamatwe na uchunguzi ufanyike na endapo itabainika amehujumu achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wahandisi wote nchini’’, amesema Aweso. 

Amesema kuwa wizara itaandaa orodha ya majina ya wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na kuikabidhi kwa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi ili wafutiwe kabisa usajili na kutopewa kazi yoyote tena nchini endapo watathibitika kufanya hivyo.

Akiwa Ulanga Naibu Waziri Aweso amezindua ofisi ya maji ya Kata ya Lupiro, mradi wa maji wa visima 27 katika Kijiji cha Chikuti, ambacho ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo na kukagua skimu ya umwagilaji ya Mnepa, iliyopo Kata ya Lupiro. 


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search