WAZIRI:Ukuta mirerani utaweka rekodi Afrika...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Simanjiro

NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Ujenzi wa Ukuta kuzunguka machimbo ya  Mirerani ni jambo la Kihistoria na kwamba linatarajiwa kuweka rekodi Barani Afrika.



Naibu Waziri Doto Biteko kulia akijadiliana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandali ya uzinduzi wa ukuta wa mirerani


Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo jana Machi 23,2018  wakati wa kikao cha Maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta huo unaotarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi Aprili na rais Dk John  Magufuli.


Ameongeza kuwa, ukuta huo ni jambo ambalo watanzania wamelisubiri kwa miaka mingi licha ya kuwepo kwa mapendekezo na sasa hatua zimechukuliwa na kutekelezwa.

Pia amelipongeza Jeshi kwa nidhamu kubwa ambayo limeonesha kwa ujenzi wa ukuta huo  wenye urefu wa kilomita 25.4  na ambao ujenzi wake umechukua kipindi cha miezi 3 tofauti na ilivyopangwa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amelipongeza Jeshi kwa kazi ambayo imefanyika na kuwataka Wajumbe wa kamati kukamilisha utekelezaji wa majukumu yote kwa wakati.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Simanjiro, Wizara ya Madini,  Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) , Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO - Manyara) na Wakala wa Barabara ( TANROAD)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search