Nondo apandishwa kortini, arudishwa mahabusu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Iringa
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa imezuia dhamana ya Mwenyekiti wa Mtandao wanafunzi vyuo vikuu, Abdul Nondo kwa sababu za usalama wake kwa madai kuwa bado maisha yake yapo hatarini na amerudishwa mahabusu.
Abdul Nondo akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Akizuia dhamana hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya Iringa John Mpitanjia amesema anaomba muda wa kupitia vifungu vya sheria hadi Machi 26,mwaka huu ili kujiridhisha maisha yake hayatakuwa hatarini kama mtuhumiwa akipatiwa dhamana.
Abdul Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni ambapo inaelezwa kuwa Machi 7 mwaka huu akiwa Ubungo alichapisha na kusambaza taarifa kwa kutumia mtandao WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Shtaka la pili ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askali katika kituo cha polisi Mafinga na kusema kuwa alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana Dar es salaam na kupelekwa kiwanda cha pareto Mafinga.
Mshtakiwa amekana mashtaka yote na amerudishwa mahabusu hadi Machi 26 atakapofikishwa tena mahakamani kwa ajili ya kusilikiliza maamuzi ya mahakama juu dhamana.
No comments:
Post a Comment