Azam FC yatupwa nje FA...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Azam
imeondolewa kwenye michuano ya FA na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati 9-8
kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex.
Mtibwa imekuwa timu
ya tatu kuingia nusu fainali baada ya Stand United iliyoitoa Njombe kwa bao
moja na Polisi Tanzania ikitoa Tanzania Prisons kwa mabao 2-0.
Mchezo huo
ulilazimika kwenda kwenye changamoto za penati baada ya kutoka sare ya bila
kufungana katika muda wa kawaida.
Azam ilicheza vizuri
zaidi kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi lakini Mtibwa wao walikuwa bora
kipindi cha pili huku wakionekana kujilinda kuliko kushambulia.
Penati za Mtibwa
zilifungwa na Hassan Dilunga, Ismail Muhesa, Stamili Mbonde, Nditi, Hassan
Isihaka, Hassan Mganga, Salum Kihimbwa, Kasian Ponera, Dickson Daud wakati
Henry Joseph akikosa mkwaju wake.
Wakati zile za Azam
zilifungwa na Himid Mao, Yahaya Zayd, Bruce Kangwa,
Agrey Morris, Joseph Kimwaga, Joseph Mahundi, Salehe Abdallah na Salum
Abubakar wakati Frank Dumayo na Abdallah Kheri wakipoteza mikwaju.
Kesho kutakuwa na
mchezo mmoja wa kukamilisha robo fainali ya michuano ambapo Singida United
itaikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Namfua.
No comments:
Post a Comment