Bavicha kula pasaka na akina Mbowe gerezani...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
VIONGOZI wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) leo
watasherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa kuwatembelea viongozi wa chama hicho
waliopo magerezani.
Patrick Ole Sosopi
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi ataongoza msafara wa
viongozi wa baraza hilo watakaokwenda Segerea kumtembelea Mwenyekiti wa Chadema
Taifa, Freeman Mbowe na wenzake.
Amesema wamefikia uamuzi huo kwa lengo la kwenda kuwatia moyo na
kuwa nao pamoja.
Amesema viongozi wengine watakwenda Mbeya kwa ajili ya Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel
Masonga.
"Tunataka kusherehekea nao Pasaka na kuwafahamisha kuwa
chama kinaendelea, hatuwezi kurudishwa nyuma wala kutetereshwa,"amesema.
Ole Sosopi pia amewataka vijana wa baraza hilo kuwa tayari
kupambana kwa ajili ya chama.
Amesema; "Kuna mambo mengi yanaendelea na tunafahamu wazi
kuna ajenda ya kutaka kukifuta Chadema, sasa nawaambia hakuna namna chama hiki
kitafutwa, tupo imara na tunazidi kuimarika,'
“Vijana kazi yetu ni kulinda chama na kazi hiyo tutaifanya kwa
nguvu zote bila woga, hatutaogopa kufa," amesema.
No comments:
Post a Comment