Chama cha wafanyakazi serikali za mitaa cha ipongeza serikali kuwarudisha watumishi la 7 kazini...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa nchini (TALGWU) kimeipongeza serikali kwa kuwarudisha kazini watumishi wa umma darasa la saba ambao waliokuwa wameondolewa.
Katibu Mkuu- TALGWU Rashid Mtima, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya serikali kpitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika kutangaza kurudishwa kwa watumishi hao na kulipwa mishahara yao ya kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa.

Akitoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam akizungumza na waandhishi wa habari, Katibu Mkuu- TALGWU Rashid Mtima amesema kwa hatua hiyo serikali imezingatia mapendekezo ya chama chao.

“Kwa niaba ya wanachama wote wa TALGWU nchini, napenda kutoa shukrani za dhati kwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Dokta  John Pombe Magufuli kwa kuzingatia mapendekezo yaliyowasilishwa na chama serikalini,” amesema Mtima.

Mtima pia ametoa shukrani kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa, waziri wa sera, bunge, kazi, ajira, vijana na walemavu Jenista Mhagama, Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo, katibu mkuu wizara ya kazi Eric Shitindi, Tamisemi Mussa Lyombe pamoja na Utumishi Dr. Laurean Ndumbaro, TUCTA pamoja na wabunge waliozungumzia suala hilo bungeni katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search