Mpenzi wa Nondo kutoa ushahidi mahakamani...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Iringa

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, Veronica Fredy anatarajiwa kuletwa makamani kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.
Abdul Nondo

Mbali na mpenzi huyo wa Nondo, Jamhuri pia inakusudia kuleta mashahidi wengine wanne ambao ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mfanyakazi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.

Kesi hiyo ilikuja leo mbele ya hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo Wakili wa Serikali, Abel Mwandalamo amesema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijini Dar Es Salaam na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Wakili Mwandalamo amedai upande wa Jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Hakimu Mpita Njia ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, kutokana na maombi ya upande wa utetezi ya Wakili Charles Luoga.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search