Dk. Mpango ateta na Mkurugenzi mtendaji Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika..soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwndishi Wetu, Washington D.C
Mikutano ya
Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia
kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo
kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma
mbalimbali kuweza kujadili hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza
umasikini.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
(wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya
Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayumo pichani) kuhusu mpango kazi wa
kuboresha uwekezaji Tanzania. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt.
Yamungu Kayandabila.
Katika
mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya
Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku
akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa
nguvu zote.
Akiendelea
kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka
mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi
wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la
Tanzania.
Pia Waziri
Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi
wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha
Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler’s Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya Mto
Rufiji.
Kupitia
miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt. Mpango
alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya Dunia ili
uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.
Kwa upande
wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew
Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada inazozionesha hasa katika
kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee na juhudi zetu za kuimarisha
uchumi wetu hususani katika sekta ya kilimo na pia amefurahishwa na hatua
mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment