Walichosema Diamond, Nandy baada ya kuhojiwa na TCRA...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASANII wa
muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul ' Diamond' na Faustina
Charles 'Nandy' kila mmoja ameonekana kujutia kitendo cha kusambaza picha chafu
mtandaoni ambazo ni kinyume na maadili ya Mtanzania huku akiwaomba vijana
kutoitumia mitandao vibaya.
Diamond na
Nandy kila mmoja kwa wakati wake walisambaza picha chafu mtandaoni hali
iliyosababisha Serikali kushindwa kuvumilia na hivyo Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam liliamua kuwakamata na kisha kuwahoji kabla ya leo
kuzungumza na waandishi wa habari wakiwa Mamakala ya Mawasiliano
Tanzania(TCRA).
Kwa upande
wa Diamond amesema anajua kitendo cha kusambaza video ambayo imekwaza wengi na
kwamba tukio hilo sasa limemfundisha kuwa anatakiwa kuwa mtumiaji mzuri wa
mtandao na si kuweka picha ambazo hazina maadili ya kitanzania na kuomba vijana
wengine kuacha tabia ya aina hiyo.
"Nikiri
binafsi ninao mashabiki wengi mtandaoni ambao wanafuatilia kila ninachokifanya
na wakati mwingine wanaiga kutoka kwangu.Niwaombe waitumie mitandao ya kijamii
vizuri kwani unaweza kufanya jambo kwenye mtandao ukadhani upo kama chumbani
kumbe ni tofauti.Mtandao hakuna tofauti na kufanya jambo barabarani kwani kila
mtu ataona.
"Kosa
la kusambaza picha chafu mtandaoni limenifanya nijifunze mambo mengi tu na TCRA
wametueleza madhara yake na kubwa zaidi sheria na kanuni ambazo ni mpya
zinazoweza kumbana anayetumia mtandao vibaya,"amesema Diamond.
Amefafanua
yeye na wasanii wengine wangi wanayo tabia ya kuamini wanaweza kufanya chochote
hasa kinachohusu sanaa ya muziki kumbe haiko hivyo kwani pamoja na kufanya
muziki bado Serikali nayo inawajibu wa kusimamia maadili yetu.Amesema anatambua
juhudi ambazo zinafanywa na Serikali katika kuhakikisha wasanii wa Tanzania
wanapiga hatua na kuwa na maendeleo yanayotokana na kazi yao lakini matendo
ambayo baadhi ya wasanii wanafanya yanaweza kukatisha tamaa viongozi
wanaopigania maslahi ya wasanii nchini.
"Kikubwa
ni vijana kuacha kutumia mitandao vibaya na kwa wasanii lazima tuunge mkono
jitihada za Serikali kwa kuwa mabalozi wa kukemea matendo mabaya yanayofanyika
mtandaoni,"amesema.Kwa upande wa Nandy ameendelea kuomba radhi kwa kitendo
cha picha zake za faragha kusambaa mtandaoni na kusisitiza haikuwa dhamira yake
na hivyo anaomba msamaha kwa Watanzania wote na hasa mashabiki wake.
"Naomba
radhi kwa kilichotokea na sikuwa na tafuta kiki kama baadhi ya watu
wanavyodhani, ni tukio ambalo haikuwa dhamira yangu, hivyo naomba
nisamehewe,"amesisitiza Nandy wakati anazungumza akiwa TCRA
No comments:
Post a Comment