Halima Mdee aachiwa kwa dhamana...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkazi Kisutu, imemuachia kwa dhamana
Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chadema Halima Mdee.
Hatua hiyo imekuja leo baada ya mbunge huyo kufikishwa na kuunganishwa
na viongozi wenzake wa chadema wakiongozwa
na mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambao moja ya kesi inayowakabili ni kufanya
maandamano ya siyo ya halali.
Hivyo Mdee amesomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko
usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka
kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na
askari kujeruhiwa.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Mahakama imempa dhamana
kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh
milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki.
Mahakama imesema haiwezi kumnyima mshtakiwa dhamana kwa
sababu aliruka dhamana ya polisi maana polisi ni taasisi nyingine na
mahakama ni taasisi nyingine, hivyo ikampatia dhamana mshtakiwa kwa masharti
tajwa hapo juu.
No comments:
Post a Comment