Magufuli aitaka Tanesco kupunguza bei ya umeme...soma habari na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS John Magufuli amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuanza kufikiria kupunguza bei ya umeme kwani nchi inatarajia kuwa na umeme mwingi.

Rais ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa  akizindua kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi awamu ya pili.

Amesema miradi yote ya umeme ukijumlisha na wa Stiegler Gauge itafikia megawati 5000 hivyo wataibana  Wizara ya Nishati ianze kufikiria kupunguza bei ya umeme.

“Muanze kufikiria namna ya kushusha bei ya umeme, mmeanza vizuri muendelee na utaratibu huo.

“Nchi ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, maji , jua, upepo, makaa ya mawe, hata nyuklia, kwa sababu tunayo madini ya uranium yanayoweza kuzalisha umeme kwa nyuklia, kwa umeme wote huo hakuna haja ya kuwa na bei ya juu, ”amesema Magufuli.

Amefafanua kuwa anayetaka kuwekeza bila kukomoa aje, lakini siyo wawekezaji wababaishaji.

Ameeleza kuwa nchi itakuwa na umeme wa kutosha,  wa uhakika na kwa gharama nafuu.

Magufuli pia alizitaja sababu za bei ya nishati hiyo kuwa ya juu ni kutokana na umeme mwingi kuzalishwa kwa kutumia mafuta (dizeli), huku baadhi ya mikataba kuwa mibovu na ya ovyo.

Ameeleza takwimu zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/16 zinaonyesha asilimia 36.6 ya Watanzania ndiyo wameunganishiwa umeme.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search