Masogange ahukumiwa miaka mitatu jela...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
VIDEO
Queen, Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ amehukumiwa na mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya sh. milioni 1.5 baada
ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na
Oxazepam.
Hukumu hiyo imetolewa leo ambapo kutokana na hukumu hiyo, Wakili
wa utetezi Nehemiah Nkoko amesema kuwa watalipa faini.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema
kuwa katika ushahidi wa kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 3,
huku utetezi ukiwa na shahidi 1.
Hakimu Mashauri amesema kuwa ameridhishwa pasina kuacha shaka
juu ya ushahidi wa upande wa mashtaka hasa kwa uthibitisho uliotolewa na Mkemia
Mkuu wa serikali kwamba mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za
kulevya.
“Kutokana na kujiridhisha na ushahidi huo, namtia hatiani
mshtakiwa kwa makosa hayo ya kutumia dawa za kulevya,”-Hakimu Mashauri
Baada ya Masogange kutoa utetezi wake, Hakimu Mashauri amesema
kuwa ameusikia utetezi wa mshtakiwa kwamba apewe adhabu ndogo, huku upande wa
mashtaka ukitaka apewe adhabu kali.
“Nimesikiliza maelezo ya pande zote, katika kosa la kutumia dawa
za kulevya aina ya Heroin namuhukumu mshtakiwa kulipa faini ya Sh.Mil 1 ama
jela miaka 2.
” Katika kosa la pili la kutumia dawa za kulevya aina ya
Oxazepam, nakuhukumh kulipa faini ya Sh.Laki 5 ama jela miezi 12,”
amesema Hakimu Mashauri.
No comments:
Post a Comment