Halima Mdee akamatwa na jeshi la polisi...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

Halima Mdee, Mbunge Kawe

Mdee amekamatwa leo alfajiri uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini inakoelezwa alilazwa kwa matibabu.

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amethibitisha  kukamatwa kwa Halima Mdee ambapo amesema; "Ni kweli amekamatwa leo Saa 9 alfajiri  Airport, akitokea Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu na sasa yupo Central."

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) huenda akaunganishwa na vigogo wengine sita akiwamo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe katika kesi inayowakabili.

Vigogo hao wengine tayari wamekwisha kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka nane.

Kukamatwa kwa Mdee kunafikisha watuhumiwa saba kati ya nane  ambao wamekwisha kuhojiwa mwingine ambaye bado na huenda anatafutwa na jeshi hilo ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search