Hatima ya Nabii Tito Aprili 13...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma leo  imepokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya "Nabii Tito" ili kujua kama ana matatizo ya akili au la.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha amethibitisha kupokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Isanga hivyo ataipitia na kutoa uamuzi Aprili 13, 2018.

“Niseme tu kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13, 2018 siku ya ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” amesema Karayemaha.

Nabii Tito ambaye hakuweza kuhudhuria kesi yake mara mbili mfululizo leo amefika mahakamani baada ya hakimu Karayemaha kutoa maagizo ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani au aletewe taarifa rasmi ya kwa nini hafikishwi mahakamani kusikiliza kesi yake.

Februari, 2018 Nabii Tito alidai mahakamani kuwa yeye ana matatizo ya akili yaliyosababisha kutaka kujiua na hivyo Mahakama kuamuru akafanyiwe vipimo vya kitabibu ili kujua kama kweli mtuhumiwa huyo ana matatizo ya akili au la.

Nabii Tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13 kesi yake itakapotolewa uamuzi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search