Mshtakiwa mwingine kuongezwa kesi ya akina Aveva, Kaburu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa na upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyan’ge ‘Kaburu‘ kwa kumuongeza mshtakiwa mwingine.
Maelezo hayo yametolewa leo, watuhumiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo baada ya kulazwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili kwa muda mrefu rais Aveva.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai amedai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, wakili Swai ameiomba mahakama ahirisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa kutaka kumuongeza mshtakiwa mmoja.

Kufuatia ombi hilo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi April 12, 2018 kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko hayo na washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji wa fedha ambazo ni Dola za Marekani (USD) 300,000.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search