Hatua ya Chadema baada ya Mdee kuwekwa mahabausu...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumpelekea daktari wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ili aweze kumcheki na kulithibitishia Jeshi la Polisi kuwa ni mgonjwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya mbunge huyo kushikiliwa na jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam mapema alfajiri ya leo akiwa Airpot alipowasili akitokea Afrika kusini kwa matibabu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema lengo ni kuthibitisha kuwa hakuwa na nia ya kukimbia kuripoti Polisi.

"Halima Mdee bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi wa kituo cha 'Centro' Jijini Dar es Salaam mpaka hivi sasa japokuwa amewaeleza ukweli kwamba ametoka kwenye matibabu na kuwaonesha vyeti vyote vya hospitali lakini bado wanaendelea kumshikiria", amesema Mrema

Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "mpaka sasa hivi hatua tulizozichukua ni kumpeleka daktari wake ili aende kumcheki na kuwathibitishia Polisi kuwa Halima kweli ni mgonjwa pia wanasheria wa chama wataelekea kituoni hapo muda si mrefu".

Halima Mdee ni miongoni mwa viongozi wa Chadema wanaotuhumiwa na Jeshi la Polisi kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali kipindi cha uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Kinondoni

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search