Kakobe naye aitwa uhamiaji kwa mahojiano...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ASKOFU Mkuu Kanisa la Full Bible Fellowship (FGBF) Zachary Kakobe ameandikiwa barua na  Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ikimwita kwa ajili ya mahojiano.

Katika barua hiyo Askofu Kakobe ametakiwa kufika katika ofisi hiyo, Jumatatu 9.4.2018 saa 4 asubuhi, na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ili kuhojiwa juu ya uraia wake.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Askofu Kakobe amethibitisha kupokea barua hiyo, na kusema kifupi tu kwamba, atakwenda kwenye mahojiano hayo.

Tukio hili linakuja baada ya sekeseke kati ya Askofu huyo na TRA, kuhitimishwa tarehe 20.2.2018, siku ambayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alipotoa taarifa kwa umma juu ya uchunguzi wao; na baadaye kusema mjadala huo umefungwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search