Kikwete amtakia kila la kheri Alikiba katika ndoa yake...soma habari kamili na matukio360...#share
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemshukuru msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba kwa kumtembelea nyumbani kwake na kusema kuwa amempa taarifa kuwa ataoa hivi karibuni.
Kikwete amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema kuwa msanii huyo ambaye sasa bado anafanya vyema na wimbo wake wa 'Seduce me' amemwambia anatarajia kuoa siku za karibuni.
"Namshukuru Alikiba kuja kunitembelea na kunitaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni. Nimempatia nasaha zangu na kumtakia kila la kheri kwa jambo hilo jema aliloamua kufanya"alisema Kikwete





No comments:
Post a Comment