Lissu kufanyiwa upasuaji mwingine...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili
11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni
ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa
Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.
Lissu ambaye ameshafanyiwa upasuaji mara kadaa katika Hospitali
ya Nairobi nchini kenya kisha Ubelgiji, amesema kwamba oparesheni hiyo ni
sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama
kitabibu.
Hii ni Kauli yake
Habari za leo popote mlipo wapendwa wangu. .
Napenda kuwajulisha kwamba ndani ya nusu saa ijayo ninaingia kwenye operesheni nyingine tena. .
Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na 'watu wasiojulikana.' Operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo. .
Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. .
Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Na hili pia litapita. .
Wasalaam.

No comments:
Post a Comment