Ummy atoa kasoro usikilizwaji wanawake waliotelekezwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Msandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kasoro aliyoiona katika zoezi la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wa kusikiliza wanawake na watoto wanaodaiwa kutelekezwa ni kutokuwa na faragha kwa watoto.
Waziri Ummy Mwalimu

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini, Ummy amesema kinachofanywa na Makonda kipo ndani ya sheria, hata watendaji wanaowasikiliza wanawake wametoka katika idara yake.

Amesema Wizara ya Afya inaunga mkono jitihada hizo, kwamba kasoro zilizojitokeza ni kwa baadhi ya wanawake waliotelekezwa kwenda na watoto na kutojali haki za kuwalinda katika hatua hizo za awali za mashtaka.

“Makonda amefanya kitu kizuri mwamko umekuwa mkubwa, ni sawa madawati yapo na ustawi wa jamii pia wapo lakini wengi wamekuwa wazito ila kwa sasa wameitikia wito kwakuwa yeye amewahimiza wanawake wenye matatizo hayo wafike kwake, kazi imekuwa nyepesi kwani hata wanaohudumia pale ni watu wetu wa Ustawi wa Jamii,” amesema Ummy.

Amesema kilichofanyika ni kama kuita kambi ambayo baadaye matokeo yatakayopatikana yatawanufaisha wanawake na ikiwa kutakuwa na ugumu kesi itakwenda mahakamani.

Hata hivyo, Ummy ametoa wito kwa wanawake wanaokwenda kutoa mashtaka yao kuhakikisha wanalinda haki za watoto wao kwa kutowaonyesha hadharani.

“Ninasema hili ni kosa la mwanamke mwenyewe, kwa mfano yule mtoto Mchina nimesikitika sana kule ni kumnyanyapaa amesambazwa mitandaoni kila mahali anazungumziwa, niwaombe Watanzania tujitahidi kuwalinda watoto hawa, tusisambaze picha zao kwa maslahi mazuri ya mtoto,” amesema Ummy. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

1 comment

  1. Mh. Waziri yuko sahihi kabisa, Walioitwa ni wanawake waliotelekezwa na wala hawakutakiwa kwenda na watoto. Kama kuna umuhimu wa ushahidi wa kuwepo kwa watoto wataelekezwa namna ya kufika nao na pia suala la usiri litazingatiwa. Hao wanawake wanaoamua kuongea na vyombo vya habari na kupigwa picha ni kwa matakwa yao wenyewe. Ushauri pia ni kwa vyombo vya habari kuhakikisha kuwa wanapofanya mahojiano kama inabidi badsi wasiwapige picha watoto

    ReplyDelete

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search