Makonda awatahadharisha watakaokaidi wito wake...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewatahadharisha wanaume wanaodhani wanaweza kukaidi wito wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewatahadharisha wanaume wanaodhani wanaweza kukaidi wito wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.
Makonda
ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano ya kipindi cha tathimini ya mchakato wa
kudai haki za watoto waliotelekezwa ambapo amesema tangu Jumatatu zaidi ya
17,000 walifika ofisini kwake na Kati ya hao 4,400 wamesikilizwa.
Amesema
kinachomfariji ni kuona idadi kubwa ya kinababa wanaofika ofisini kwake
wanakubali kumlea mtoto ambapo hadi sasa familia 295 zimekubali kuhudumia mtoto
na familia 29 zimepima DNA.
Hata
hivyo Makonda amesema baada ya zoezi hilo ataunda tume ya kuangalia
changamoto zilizopo katika sheria ya matunzo ya mtot kisha kuifikisha kwa
waziri husika kwaajili ya kufikishwa Bungeni kwaajili kufanyiwa marekebisho.
Pamoja
na hayo Makonda amesema hatoyumbishwa na baadhi ya watu wasiojua uchungu
wanaopata kinamama kwa kubeza zoezi hilo kwakuwa yeye ametambua Mateso
waliyokuwa wakipata kinamama waliotelekezwa.
Makonda
amesema ikitokea mwanamke aliefika ofisini kwake na kumshitaki mwanaume
aliezaanae kisha uchunguzi ukafanyika na kubaini udanganyifu mwanaume anayo
haki ya kufungua kesi ya kudhalilishwa na afisa ustawi wa jamii wa mkoa
atalazimika kuwa shahidi mahakamani.
No comments:
Post a Comment